Sunday 23 November 2014

Mauaji yanalenga kuzua uhasama wa kidini mombasa


Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga kusababisha vita vya kidini nchini kenya.

Kwenye mahojiano na shirika la utangazaji la uingereza  BBC Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri ambao hawangeweza kukariri Koran.
Al Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani wa Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.

No comments: