Wednesday 26 November 2014

Messi ndiye mchezaji bora wa kandanda

Lionel Messi celebrates scoring against Apoel NicosiaNyota wa Barcelona Lionel Messi amesifiwa kuwa "mchezaji bora zaidi katika historia ya kandanda", anasema rais Josep Maria Bartomeu.
Raia huyo wa Argentina,mwenye umri wa miaka 27,ndiye mfungaji bora wa muda katika ligi ya Hispania La Liga na mabao 253 kufuatia yeye kufunga mabao matatu Jumamosi waliposhinda 5-1 dhidi ya Sevilla.
Bartomeu alisema: "Tutakuwa naye Leo hapa kwa miaka mingi ijayo, tuna furaha na kile amepata.
"Tulijua rekodi ingelikuja. Imenifurahisha sana kumwona akiisawazisha, kwa ajili yake na kwa ajili ya klabu."
Messi aliyetuzwa mchezaji bora zaidi duniani kwa miaka minne amefunga mabao 368 kwa jumla akiichezea Barcelona, klabu yake ya pekee kama mwandamizi, na mabao 45 akichezea Argentina.
Messi - ambaye pia anashikilia rekodi ya mfungaji bora katika historia ya Ligi ya Mabingwa na mabao 71 - hivi karibuni alisema kuwa mustakabali wake ni "mgumu", lakini baba yake akakataa.
Bartomeu alisema: "Hakuna maneno ya kuelezea kile anachokifanya.Anafurahi kuchezea Barcelona ambapo amekuwa kwa miaka mingi, na anapatana vizuri na wachezaji wenzake.
"Ana wasiwasi kuhusu masuala yasiyo ya michezo lakini klabu inamsaidia. Watu wanapaswa kuzungumza naye kuhusu kandanda badala ya mambo mengine."
Baada ya mchezo,kocha mkuu wa Barcelona Luis Enrique alisema anadhani Messi atapanua rekodi, ambayo hapo awali alisimama tangu mwaka wa 1955, kiasi ya kwamba itakuwa ngumu kufikiwa na mtu mwingine.

No comments: