Thursday 13 November 2014

Yanga huenda yanga ikawakosa Niyonzima,Kaseja, na Twite

kaseja
Niyonzima
Huenda klabu ya Yanga ikawapoteza wachezaji wake watatu, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Juma Kaseja raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Niyonzima, kwa upande wake amekuwa akidai kutofurahia maisha anayoishi ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
Kiungo huyo raia wa Rwanda ambaye mkataba wake unafikia ukingoni, amesema kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia klabu hiyo.
Tayari, kiungo huyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine anayotaka kwenda kuichezea kutokana na mkataba wake kubakiza miezi sita.
Katika mazungumzo yake na gazeti hili, ameeleza kushangazwa na kitendo cha kocha Marcio Maximo kumtoa kipindi cha pili bila kuambiwa sababu ili ajirekebishe kwenye mechi nne mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya Stand United, Kagera, Simba, na Mgambo.
“Mimi ni mchezaji, ninaitumikia timu yangu ya taifa (Amavubi), pia ni tegemeo katika timu hiyo, ninacheza dakika 90, sasa iweje hapa Yanga natolewa kipindi cha pili?” Alihoji.
“Kitu kingine kinachonichosha Yanga ni uzushi, ule ninaosambaziwa na baadhi ya wanachama (makomandoo) kuwa Kaseja ananishawishi nisaini Simba, kwa kuwa tunalala chumba kimoja tunapokuwa kambini,” alisema Niyonzima.
Mbali na Niyonzima, pia klabu hiyo huenda ikamkosa kipa Kaseja ambaye hajadaka mechi kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.
Inadaiwa kuwa kipa huyo yupo mbioni kurejea timu yake ya zamani, Simba ikiwa ni pamoja na Mbuyu Twite ambaye naye amegoma kusaini mkataba hadi pale uongozi utakampomtimizia masharti yake. Twite, amebakiza miezi sita kaitka mkataba wake wa kuichezea Yanga.

No comments: