Tuesday 18 November 2014

Yanga wanyakuwa Straika toka Mgambo Shooting Tanga

KOCHA wa Yanga, Marcio Maximo, amewaambia viongozi kwamba anamtaka mmoja wa mastraika wawili wa Mgambo Shooting ya Tanga,Fully Maganga au Busungu Balimi.
Maganga anashikilia rekodi ya kuwafunga vigogo Simba na Yanga msimu uliopita na alipata zawadi ya kuwa mchezaji mwenye nidhamu msimu wa mwaka juzi akajizolea Sh5 milioni.
Usajili wa Busungu ambaye si mwanajeshi unakwenda sawa licha ya kubakiza mkataba wa miezi saba na Maganga ambaye ni mwanajeshi ndiyo mipango zaidi inafanyika, lakini mpaka kufikia wikiendi hii kitakuwa kimeshaeleweka.
Kiongozi wa juu wa Yanga amewaambia waandishi wa habari  kuwa Maximo amewaweka wachezaji hao kwenye orodha yake na anataka kumpata mmoja wao na hata kama ikiwezekana wasajiliwe wote kwa mpigo.
“Upande wa Busungu mambo yanakwenda vizuri lakini utata upo kwa Maganga ambaye ni mwanajeshi kumtoa hapo ni kazi,”alisema kiongozi huyo na kufafanua mbali na kupendekezwa na benchi la ufundi sasa, juhudi za kuwafuatilia zilianza mapema tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Balimi anasifika kwa akili ya kukokota mpira, kumiliki na kutengeneza mabao ingawa Maganga ni mjanja na amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake.
Yanga inafikiria kupukutisha wachezaji watano wazalendo na kuongeza wengine ili kuchangamsha timu hiyo itakapoendelea na mechi za mzunguko wa kwanza Desemba 26.

No comments: