Friday 19 December 2014

Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2015 yatangazwa

Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza  mwakani  kutokana na matokeo ya darasa la saba  ambapo wanafunzi  427,60 kati ya  844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika .
Jumla ya wanafunzi  844,938 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na mwaka jana.
Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu huyo wa Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa hilo la saba hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.

No comments: