Friday 16 January 2015

Kocha wa Atletico adai Torres ni dume la shoka

Torres akifunga
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema Fernando Torres amerejea kuwa ''mwanaume'' ndivyo alivyomuita hivyo baada ya mshambuliaji huyo kufunga magoli yake ya kwanza tangu alipojiunga na Atletico madrid.
Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Torres alijiunga na Liverpool mwaka 2007.
Torres alijiunga na Atletico mwanzoni mwa mwezi huu na aliifungia klabu hiyo magoli mawili katika dimba la Bernabeo na kutoka sare ya mabao 2-2 ilipokutana na Real Madrid katika michuano ya Copa del rey
Torres naye ameonesha furaha yake na kushukuru wapenzi wake kwa kumuunga mkono.

No comments: