Monday 12 January 2015

Mchungaji auwawa Kanisani Huko Mombasa

Polisi akiwa ndani ya kanisa moja Mombasa baada ya kutokea shambuliziWatu wenye silaha wasiofahamika walimfyatulia risasi na kumuuwa mchungaji mmoja wakati wa ibada kanisani siku ya jumapili katika mji wa Mombasa nchini Kenya  maahala ambako polisi wanapambana na vijana wa ki-islam wenye msimamo mkali.
 
Mauaji hayo yalitokea ndani ya mlango mkuu wa kuingilia kwenye kanisa la Maximum Revival Centre katika mtaa wa majengo. Mashahidi wanasema polisi waliwazuia watu wenye silaha kuingia ndani ya kanisa na kuuwa waathirika Zaidi. Kenya imeshambuliwa mara kadhaa kwa matukio yanayohusishwa na ugaidi ikiwemo la Westgate mall  Watu hao wenye silaha hawajafahamika  lakini kundi la wanamgambo wa Al-Shabab kutoka nchi jirani ya Somalia limeshambulia malengo kadhaa nchini Kenya. Kundi hilo la Al-Shabab liliapa kulipiza kisasi kwa majeshi ya Kenya kuwepo nchini Somalia kwa ajili ya kusaidia  wanajeshi wa serikali dhidi ya wanamgambo hao.

No comments: