Thursday 22 January 2015

Samatta afanikiwa kufuzu Mtihani wa kwanza CSKA Moscowo, TP Mazembe yawapa siku Mbili kuka,ilisha usajili wake


BAADA ya mshambuliaji Mbwana Samatta kuvuka mtihani wa kwanza wa kusaka ulaji ndani ya timu ya CSKA Moscow ya Urusi, sasa timu hiyo imepewa siku mbili kati ya leo au kesho ihakikishe inamalizia taratibu za kumsajili.
Samatta hivi sasa anaendelea na mazoezi ndani ya kikosi cha timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Urusi, ambapo blogi hili ndiyo ilikuwa ya kwanza kuripoti taarifa za mshambuliaji huyo kutimkia nchini Hispania kusaka ulaji CSKA na timu nyingine za Hispania, Italia na Uswisi.
CSKA inayoshiriki kila mwaka michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, imeweka kambi jijini Campoamor, Hispania kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Urusi, ambapo inashika nafasi ya pili kwa pointi 34 nyuma ya Zenit inayoongoza kwa pointi 41.
Taarifa zilizolifikia MTANZANIA jana kutoka kwa mtu wa karibu na mchezaji huyo zimeeleza kuwa kwa sasa Samatta ameshamaliza hatua ya kwanza ya majaribio yake, taratibu zikizobakia ni timu hiyo kuanza mazungumzo ya kumsajili, huku CSKA ikipewa siku mbili za kuhakikisha inakamilisha taratibu za kumsajili.
Kama CSKA ikishindwa kwenda na huo muda, Samatta atakwenda kwenye timu nyingine kubwa zilizovutiwa naye, kwani tunataka kuhakikisha Samatta awe amepata timu Ulaya kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili linaloendelea huko,” kilieleza chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa jina
Katika hatua nyingine, chanzo hicho kiliongeza kuwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Hispania, Atletico Madrid kupitia wasaka vipaji wao wamevutiwa na Samatta, sambamba na timu moja ya Ujerumani.
“Tunapambana na muda huku, hivyo kama CSKA wasipokamilisha dili kwa muda huo, tutahamia kwa timu mbili za Hispania zinazomuhitaji ikiwemo Atletico Madrid yenye nyota kama Fernando Torres, Mandzukic na Koke na timu moja ya Ujerumani na nyingine kutoka Italia na Uswisi,” kilieleza.
Samatta anayechezea timu ya TP Mazembe ya DR Congo, amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya kikosi hicho, ambapo mmiliki wake, Moise Katumbi, naye ameridhia kuuzwa kwa mshambuliaji huyo hatari waliyemsajili mwaka 2011 akitokea Simba kwa dau la Dola za Marekani 150,000.

No comments: