Friday 9 January 2015

Yanga yasitisha Mkataba na Juma Kaseja

Juma Kaseja.
YANGA SC imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango Juma Kaseja, iliyemsajili kwa Sh. Milioni 40 Novemba 8, mwaka juzi.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari leo katika hoteli ya Zanzibar Ocean View visiwani hapa kwamba, hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kuanza kujiengua katika timu.


“Tumefikia uamuzi wa kuachana na Kaseja, baada ya yeye mwenyewe kuanza kujiengua katika timu,”amesema Muro.
Mwishoni mwa mwaka jana, Kaseja aliwasilisha barua kwa mwajiri wake, Yanga SC kutoa taarifa ya kuvunja makataba wake, uliokuwa umebakiza mwaka mmoja.
Katika barua yake, Kaseja alisema sababu ya kuvunjwa Mkataba huo ni kukiukwa kwa masharti yaliyokubaliwa wakati wa kusainiwa Novemba 8, mwaka jana.
Barua ya Kaseja iliyotumwa kupitia wakili wake, Mbamba & Co Advocates, Kaseja imesema wakati wa kusainiwa Mkataba huo ilikubaliwa malipo ya Sh. Milioni 40 yafanyike kwa awamu mbili.
Alisema awamu ya kwanza, alilipwa Sh. Milioni 20 baada ya kusaini Mkataba huo, na ikakubaliwa fungu lililobaki apatiwe Janauri 15, mwaka jana na kwa sababu malipo ya fedha ndio msingi wa Mkataba wenyewe, kushindwa kulipa fedha hizo kunaondoa uhalali wake.hivyo, Yanga SC baadaye ilikuja kusema imekwishamlipa fedha zake zote Kaseja na hana anachodai, ingawa kipa huyo alifungua madai mapya, akidai anachukiwa na kocha wa makipa, Juma Pondamali hivyo hana amani ya kufanya kazi.

REKODI YA JUMA KASEJA YANGA SC
Yanga SC 3-2 KMKM (Kirafiki, alifungwa mbili Dar)
Yanga 1-3 Simba SC (Mtani Jembe, alifungwa tatu Dar)
Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki, hakufungwa)
Yanga SC 3-0 Ankara Sekerspor (Ziara ya Uturuki, hakufungwa)
Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki, alifungwa mbili)
Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa, hakufungwa)
Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu, hakufungwa)
Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu alifungwa mbili)
Yanga SC 1-0 Chipukizi (kirafiki Pemba, hakufungwa)
Yanga SC 2-0 KMKM (Kirafiki Zanzibar, hakufungwa)
Yanga SC 0-0 CDA (Kirafiki Dodoma, hakufungwa)
Yanga SC 1-0 Ambassador (Kirafiki, hakufungwa)

No comments: