Wednesday 11 March 2015

Biashara ya Kuuza watoto yashamiri China


Uchunguzi wa BBC umegundua kuwa watoto wanawekwa katika matangazo ya kuuzwa kupitia kwa mitandao nchini China licha ya kuwepo kwa jitihada za polisi za kupambana na ulanguzi wa watoto.
Mojawapo ya matangazo hayo ni lile la mtoto wa umri wa miezi minane aliyekuwa akiuzwa kwa dola 30,000.
Mchunguzi wa  wa shirika la utangazaji la Uingereza BBC aliyejifanya kuwa mnunuzi alionyesha mtoto kupitia kwa video ya mtandao na mwanamke ambaye alisema kuwa hangeweza kukidhi mahitaji ya kumlea mwana huyo.
Licha ya hatua ya kutangazwa kwa watoto mitandaoni kuwa halali nchini China, matangazo ya watoto ili kuwauza ni haramu .

No comments: