Monday 18 May 2015

Ahukumiwa jela miaka 30 kwa kumbaka mlemavu wa Akili



Image result for mahakamaMtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Shedrack Saita mkazi wa kata ya Musa kijiji cha Likamba mkoani Arusha mwenye umri wa Miaka 53 amehukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la kumbaka Msichana Mwenye ulemavu wa akili.
Hukumu hiyo imetolewa jana katika mahakama ya wilaya ya Arumeru iliyoko mkoani Arusha jana
Hakimu ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kwamba “msichana aliyebakwa alifahamika kwa jina la Esuphati, mwenye umri wa miaka 16 mlemavu wa akili” alibakwa tarehe 27.7.14 kwenye shamba la mahindi
Hata hivyo hakimu huyo ameongeza kwa kusema “mtuhumiwa alipokamatwa kwa mara ya kwanzaalikiri kuhusika na tukio hilo na kuiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hakudhamiria kubaka kwani ni pombe ilimshawishi kufanya hivyo .

No comments: