Tuesday 5 May 2015

Bilionea wa Kinigeria ataka kuinunua Arsenal

Aliko Dangote
Mtu tajiri barani Afrika Aliko Dangote amesema kuwa bado anataka kuinunua kilabu ya Arsenal licha ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2010 alipotaka kununua hisa za kilabu hiyo.
Bilionea huyo kutoka Nigeria ni tajiri mara nane ya alivyokuwa wakati alipojaribu kununua hisa za klabu hiyo na kwamba shabiki huyo wa Arsenal bado hajatupilia mbali ndoto yake ya kutaka kuinunua kilabu hiyo ya Landon Kazkazini.
''Bado nina matumaini kwamba siku moja nitainunua timu hiyo',' alisema Dangote mwenye umri wa miaka 58.''Naweza kuinunua bei ambayo wamiliki wake itakua vigumu kukataa'', huku akiongezea kuwa ''najua mpango wangu''.
Uwanja wa Emirates
La kushangaza ni kwamba Dangote ametaja hadharani kwamba Arsene Wenger anafaa kubadilisha mbinu yake akisema kuwa timu hiyo inahitaji mwelekeo mpya.
Dangote ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 ni tajiri zaidi ya Stan Kroenke ambaye anamiliki hisa nyingi katika kilabu hiyo na Bilionea raia wa Uzbek Alisher Usmanov ambao wamekuwa wakipigania udhibiti wa kilabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

No comments: