Sunday 24 May 2015

Kikosi bora cha msimu VPL hiki hapa

Kikosi bora cha Ligi ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/15Baada ya kila timu kucheza mechi 26,mtandao wa Goal umetangaza  kikosi bora cha wachezaji 11 na wale wa akiba kufuatia mchango wa wchezaji hao kwenye timu zao
LIGI ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/15 imemalizika Jumamosi ya Mei 9 huku klabu ya Yanga ikinyakua ubingwa huo kwa kuwavua ubingwa timu ya Azam FC ambayo ilikuwa bingwa kwa mara ya kwanza msimu uliopita tangu ilipoanza kushiriki ligi hiyo misimu nane iliyopita.
Jumla ya timu 14 zilishiriki Ligi hiyo iliyokuwa na msisimko mkubwa ukilinganisha na misimu mingine iliyopita na kushuhudiwa timu mbili zinazo milikiwa na Majeshi za Ruvu Shooting na Polisi Moro zikishuka daraja kucheza ligi raja la kwanza msimu ujao.
Baada ya kila timu kucheza mechi 26, mtandao wa Goal unakuletea kikosi bora cha wachezaji 11 na wale wa akiba kufuatia mchango wa wchezaji hao kwenye timu zao.

1.Ally Mustapha ‘Barthez’ (Yanga)
Huyu ni kipa aliyefungwa mabao machache kutika mechi nyingi alizoidakia Yanga msimu huu na kuipa ubingwa wa pili tangu alipojiunga nayo misimu mitatu iliyopita akitokea kwa mahasimu zao Simba.
Barthez anastaili kuwa kipa namba moja siyo tu kwa kufungwa mabao machache lakini hata uvumilivu wake kwenye kikosi cha Yanga baada ya kuwa kipa chaguo la tatu baada ya Deogratius Munishi ‘Dida’ na Juma Kaseja lakini alipambana hadi kurudishwa kuwa namba moja na kufanya kazi kubwa ikiwemo kwenye michuano ya kimataifa na kunawakati alicheza mechi nane za ligi ya Vodacom msimu huu bila kufungwa hata bao mojaa.

2.Hassan Ramadhan ‘Kessy’ (Simba)
Kessy ni kati ya mabeki anayestaili kuwepo kwenye kikosi bora cha msimu huu kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa klabu yake ya Simba licha ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Sifa kubwa ya Kessy siyo kuzuia bali pia amechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mabao ya Simba kupitia krosi zake ambazo mara nyingi zimekuwa na matunda zinapo wafikia washambuliaji wake kama Emmanuel Okwi au Ibrahim Ajibu.

3.Oscar Joshua (Yanga)
Pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuuchezea mpira na kupiga chenga lakini Oscar ametoa mchango mkubwa kwenye ubingwa wa Yanga msimu huu.
Oscar aliyecheza mechi 21 za ligi ya Vodacom msimu huu amefanya kazi kubwa ya kuzuia na kupandisha mashambulizi mbele kwa kupiga krosi huku wakati mwingine washambuliaji wa timu pinzani wakishindwa kutumia upande wake kutokana na uchezaji wake wa kutumia nguvu nyingi , beki huyu aliweza kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia kule Sousse wiki moja na nusu iliyopita.

4.Pascal Wawa (Azam FC)
Huyu ni beki mpya kwenye ligi ya Vodacom lakini mchango alioutoa kwa muda mfupi akiwa na klabu ya Azam unamfanya aingia kwenye kikosi hiki cha Goal msimu huu.
Pamoja na kushindwa kuisaidia Azam kutetea ubingwa wake lakini Wawa amefanya kazi kubwa kwenye kikosi hicho kwa kutumia uzoefu wake kuwadhibiti washambuliaji watukutu na hilo lilijionyesha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo katika mchezo wa kwanza dhidi ya El Merreikh ya Sudan aliofanya kazi kubwa siku hiyo na kuokoa hatari nyingi.
5.Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga)
Beki tegemeo wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefanya kazi kubwa mno katika kuipigania timu yake msimu huu na kufanikiwa kuipa ubingwa wa 25.
Cannavaro mbali ya kujitolea kwa ajili ya Yanga lakini amekuwa akifanya jitihada kubwa za kupande mbele na kufunga mabao ambayo yameisaidia timu hiyo kutangaza ubingwa mapema kabla ya mechi mbili za mwisho.
6.Salum Telela (Yanga)
Licha ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara lakini Telela amekuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya klabu ya Yanga msimu huu kutokana na kazi yake kubwa aliyoifanya katika mechi chache alizoichezea klabu hiyo.
Kukosekana kwa Telela kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du Sahel, kulionekana kuiangusha Yanga kwenye eneo la kiungo na kusababisha wapinzani kupenya mara kwa mara huku Hassan Dilunga akishindwa kuhimili vishindo vyao.

7.Simon Msuva (Yanga)
Msuva anaweza kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu kwa jinsi alivyocheza kwa kiwango cha juu. Kwanza ameisaidia timu yake kuwa bingwa na pia ameibuka mfungaji bora wa ligi akiwa amefunga mabao 17.
Msuva alikuwa mmoja ya wachezaji wachache wanao ogopewa na timu pinzani na hiyo imechangia sana hata kupata timu ya kuichezea nchini Afrika Kusini kutokana na kiwango alichokuwa nacho kwa sasa licha makosa madogo madogo ambayo kunawakati yalimweka kwenye kipindi kigumu.

8. Haruna Niyonzima (Yanga)
Inasemekena ndiye kiungo aliyetoa pasi nyingi za mabao katika timu ya Yanga msimu huu. Kocha wake Hans Pluijm alikuwa akimchezesha kama winga wa kushoto na mara nyingine kiungo. Hata hivyo alimudu kucheza nafasi yake mpya ya winga na kushirikiana vizuri na wenzake jambo lililoisaidia sana timu hiyo kuweza kutoa vipigo kila mara katika michezo yake.

9.Amisssi Tambwe (Yanga)
Ukitaka mashabiki wa Simba wakuchukie litaje jina la Tambwe mbele yao kwani wanaijua shughuli yake na wamekuwa kila mara wakiulaumu uongozi wa timu yao kwa kumuacha mchezaji huyo mzuri. Tambwe alijiunga na Yanga wakati wa dirisha dogo akitokea Simba na katika kipindi hicho kifupi aliifungia Yanga mabao 13 kwenye ligi ya Vodacom na kumaliza nafasi ya pili nyuma ya mchezaji mwenzake wa Yanga Simon Msuva.
Tambwe ambaye ndiye mfungaji bora msimu uliopita akiifungia Simba mabao 19 ametoa mchango mkubwa kwa Yanga siyo tu kwenye ligi ya Vodacom bali hata kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo amefunga mabao matatu yakiwemo yote mawili katika mchezo wa kwanza dhidi ya BDF XI ya Botswana na bao moja dhidi ya FC Platinum FC ya Zimbabwe.
10. Didier Kavumbagu (Azam)
Huyu ndiyo kinara wa mabao kwenye klabu ya Azam FC akiwa na mabao 10 huku ukiwa ndiyo msimu wake wa kwanza tangu ajiunge nayo akitokea Yanga.
Kavumbagu amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Azam na hata kufikia hatua uongozi wao kumungezea mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao

11.Emmanuel Okwi (Simba)
Nyota huyu ni mzee wa kubadili matokeo wakati wowote. Okwi anajiamini na ndiyo mchezaji ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa Simba kumaliza ligi katika nafasi iliyopo kwa ajinsi anavyocheza kwa kujituma uwanjani.
Okwi amekuwa akiipatia ushindi timu yake hata pale inapokuwa katika wakati mgumu. Katika msimu huu alikuwa akikosekana Okwi timu ya Simba ilikuwa inayumba katika safu ya ushambuliaji.
Wachezaji wa Akiba
Aishi Manula (Azam)
Mbuyu Twite (Yanga)
Mudathir Yahaya (Azam)

Mrisho Ngassa (Yanga)

Raphael ALpha (Mbeya City)
Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
Ibrahim Ajibu (Simba).

No comments: