Thursday 21 May 2015

Polisi auwa mwanajeshu nchini Burundi

Mwanajeshi auawa na askari polisi Bujumbura
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na mashahidi jijini Bujumbura ni kwamba askari polisi mmoja alimfyatulia risasi mwanajeshi mmoja na kusababisha mwanajeshi huyo kufariki.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika kitongoji cha Nyakabiga ya 3 mtaa wa 9 jirani na mgahawa uitwao Niwakal.
Pacifique Nininahazwe, mmoja wa watu waliotoa wito wa maandamano dhidi ya muhula wa 3 wa rais Nkurunziza katika uchaguzi wa mwezi Juni nchini Burundi.
Inakaribia wiki nne tangu maandamano hayo kuanza jijini Bujumbura.
Taarifa zinafahamisha kuwa takriban wanajeshi 12 walifariki tangu kuendeshwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali ya rais Nkurunziza.
Jijini Bujumbura kumeripotiwa maandamano kwa mara nyingine ambapo mtaani Musaga mtu mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi.
Ifahamike kuwa rais Pierre Nkurunziza amesaini kuahirishwa kwa muda wa wiki moja uchuguzi wa wabunge nchini Burundi

No comments: