Monday 25 May 2015

Waziri mkuu wa uturuki apiga Hat trik

Waziri Mkuu wa Uturuki apiga Hat-Trick!Davutoglu afunga goli 3 katika dakika 40 alizocheza kwenye mechi ya kirafiki

Wazir Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, alijumuika na wachezaji wa zamani wa kilabu ya Trabzonspor katika mechi maalum ya kirafiki iliyochezwa mjini Trabzon nchini Uturuki.
Davutoglu aliyeingia uwanjani na jezi nambari 61 mgongoni, alikaribishwa na kupewa maua uwanjani kwa heshima.
Kabla ya mchuano huo kung’oa nanga, Waziri Mkuu Davutoglu pia alipiga picha za ukumbusho na wachezaji wa zamani wa kilabu ya Trabzonspor.
Mechi hiyo ilidumu kwa dakika 40, zilizogawanywa katika dakika 20 kila kipindi na kumalizika kwa sare ya 4 – 4.
Davutoglu aliweza kuifungia timu yake goli 3 katika mechi hiyo na kutoa pasi moja iliyozalisha goli.

No comments: