Wednesday 13 May 2015

Waziri wa Ulinzi auawa kwa kusinzia mbale ya Rais

Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alipigwa na kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa wakuu serikalini
Idara ya ujasusi ya Korea Kusini imesema kuwa waziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alikutana na mauti yake baada ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi Aprili.
Bwana Hyon anasemekana kuwa alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na rais Kim jambo lililomuudhi sana kiongozi huyo wa kiimla.
Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa serikali ya Korea Kaskazini.
Waziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
Bwana Hyon alipandishwa cheo na kuwa Generali mwaka wa 2010 na kuuawa kwake kunatia shaka udhabiti wa uongozi wa rai Kim Jong -un.
Hyon alipandishwa cheo na kutangazwa kuwa waziri wa usalama wa taifa mwaka uliopita.
Mwandishi wanaanasema mauaji hayo ya kikatili mbele ya umma ikiwa yatathibitishwa, yanaonyesha athari za uasi dhidi ya Kim Jong-un.
Mapema idara hiyo ya ujasusi ilisema viongozi wakuu katika serikali ya Korea Kaskazini wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.

No comments: