Wednesday 17 June 2015

Ban-ki Moon aonyesha wasiwasi kuhusu hukumu ya Morisi

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki- Moon amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusu misri kuthibitisha adhabu ya kifo.
Adhabu hiyo ni dhidi ya rais aliyepinduliwa Mohamed Morsi, na watu wengine zaidi ya 90 kwa kuhusika na utorokaji wa jela mwaka 2011.
Umoja wa mataifa unapinga matumizi ya adhabu ya kifo katika mazingira yoyote, ilisema ofisi ya bwana Moon, katika taarifa yake jana Jumanne.
Imesema katibu mkuu ana hofu kuhusu uamuzi huo, uliotolewa baada ya kesi ya pamoja ambayo inaweza kuleta mtazamo tofauti kwa uthabiti wa muda mrefu nchini misri.

No comments: