Wednesday 17 June 2015

Hong Kong kujadili mageuzi ya kisiasa

Hong Kong
Baraza la kikatiba la Hong Kong limeanza kujadili mpango wa mageuzi ya kisiasa kabla ya kupigiwa kura baadaye wiki hii.
Mapendekezo yao ni kuwa wakaazi wa Hong Kong wataweza kumpigia kura kiongozi wao katika uchaguzi wa mwaka wa 2017 japo wagombea wote kwanza lazima waidhinishwe na serikali kuu ya China .
Watetezi wa demokrasia wameshutmu hilo kuwa demokrasia ya longo longo.
Tayari mamia ya watetezi hao wamekusanyika nje ya afisi za baraza hilo wakibeba mabango na kutoa maneno ya kutukana baraza hlo.
Lakini wanaoungamkono mpango huo kutoka Beijing wanasema kuwa Hong Kong kwa sasa inahitaji uthabiti na wametoa wito kwa wabunge hao wapitishe pendekezo hilo.
CHANZO; BBC SWAHILI

No comments: