Tuesday 23 June 2015

Jonas mkude atimkia Afrika kusini kwa majaribio

mkude-768x403
Kiungo wa Klabu ya Simba Jonas Mkude anatarajiwa kwenda Afrika Kusini  Alhamisi Juni 26 mwaka huu kwa majaribio ya wiki mbili katika Klabu ya Bidvest Wits.
Akiongea na tovuti ya Simba, Mkude alisema fursa hii ni adimu na anaamini akifanikiwa ataiwakilisha vyema Simba na Tanzania kwa ujumla. 
Akizungumzia pengo litakaloachwa ikiwa atafanikiwa majaribio alisema “pengo langu linaweza kuzibwa kwani Simba ina wachezaji nyota wanaojituma na wenye uwezo”
Alitumia mahojiano hayo kuwaasa vijana mbalimbali wanaotaka kufanikiwa katika soka kujituma na kuwa na nidhamu ili kupata mafanikio na kukuza vipaji vyao.
Raisi wa Simba Evans Aveva alisema “Simba inamtakia kila la kheri Mkude kwenye majaribio yake kwenye Klabu ya Bidvest Wits huko Afrika Kusini na hili liwe ni fundisho kwa vijana wengine kuendeleza vipaji ili waweze kucheza mpira kwenye ligi za Nchi nyingine kubwa hivyo kukuza upeo na vipaji zaidi katika soka”.
Mkude ni zao la ukuzaji wa vipaji vya Klabu ya Simba inaotilia mkazo kwani ni chipukizi aliekulia katika mfumo wa Simba wa uendelezaji vipaji.
Mkude alizaliwa Desemba 3, 1992 Kinondoni B na kuanza soka lake akiwa mlinda mlango hadi kuwa kiungo wa kutegemewa. Aidha alianza elimu ya msingi mwaka 1998 katika shule ya Hananasif na kumaliza mwaka 2005.

No comments: