Saturday 20 June 2015

Maafisa uandikishaji BVR wazuia waandishi wa ITV kupiga picha wahamiaji haramu kuficha ukweli

Siku moja baada ya ITV kutangaza kundi kubwa la wahamiaji haramu wakijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa ELECTRONIC BVR wakishawishi watendaji wa serikali kwa kuwapatia rushwa ya fedha na mifugo baadhi ya maafisa uandikishaji wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wameizuia kwa muda kamera ya ITV kupiga Picha wahamiaji haramu wakitaka kuonyeshwa kibali kutoka tume ya taifa ya uchaguzi kinachoruhusu mwaandishi wa habari kufanya kazi za uchunguzi.

Mgogoro huo umetokea kwenye kituo cha uandikisha cha bomani karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya,makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Karagwe na kituo cha polisi kayanga ambapo ITV ilibaini kuwepo kwa kundi la wahamiaji haramu wakijiandikisha kinyume cha sheria na ilipofika kwenye eneo la tukio na kupiga picha waliibuka maafisa uandikishaji wakazuia eneo hilo kupigwa picha kati ya mwandishi na afisa uandikishaji kituo cha bomani kufuatia sakata hilo ITV ikazungumza na mawakala  wa vyama vya kisiasa ambao wame bainisha jinsi maafisa uandikishaji wanavyo ruhusu wahamiaji haramu kujiandikisha kwa njia ya rushwa kinyume cha sheria za nchi.
 
Alipotakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili maafisa uandikishaji afisa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya karagwe Bi.Ashura Kajuna ametofautiana maelezo na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Karagwe mhandisi Richard Luyango juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili watumishi wa serikali.

No comments: