Tuesday 16 June 2015

Mahakama yamhukumu Morisi Kunyongwa

Mahakama ya Misri imemhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa nchini hiyo Muhammad Morsi
Mahakama ya juu ya Misri imehakiki hukumu ya mahakama ya chini ya kumnyonga rais wa zamani Muhammad Morsi kwa makosa ya kupanga njama ya kuwatorosha wafungwa katika kipindi cha maandamano ya kumng'oa madarakani rais aliyekuwepo Hosni Mubarak mwaka wa 2011.
Hukumu hiyo inafuatia majadiliano baina ya majaji wa mahakama kuu na kiongozi wa kidini Mufti.
Awali mahakama ya chini ilikuwa imemhukumu kifungo cha maisha Morsi, kwa kosa la kufanyia ujasusi kundi la Kipalestina la Hamas, kundi la wapiganaji la Hezbolah na Iran.
Viongozi wengine 16 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood , akiwemo kiongozi wao Khairat el Shater,walihukumiwa kifo.
Bwana Morsi pia anakabiliwa na hukumu tofauti ya kifo baada ya kupatikana na kosa la kushiriki katika kupanga njama ya kutoroka gerezani zaidi ya miaka minne iliyopita, wakati mtangulizi wake Hosni Mubarak alipopinduliwa.
nullMorsi tayari amehukumiwa kunyongwa
Mahakama inatarajiwa kutoa hukumu ya mwisho juu ya kesi hiyo baada ya mapumziko mafupi.
Mahakama imekuwa ikisubiri ushauri maalumu kutoka kwa kiongozi Mkuu wa Kidini nchini humo Mufti.
Kundi la Muslim Brotherhood lilitaja hukumu hiyo kama upuzi mtupu.

No comments: