Wednesday 17 June 2015

Majambazi Yaua Dar baada ya kujibizana kwa risasi na Polisi kwa muda


MAJAMBAZI watatu wameuwawa katika matukio mawili tofauti Jijini Dar es Salaam, likiwamo la majambazi wawili kufariki dunia baada ya kujibizana  kwa risasi na Polisi.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simoni Sirro, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Mbagala Charambe wakiwa na silaha mbili ambazo ni Mark IV yenye namba 308139 ikiwa na magazine yenye risasi sita.
 
Alisema majambazi hayo pia walikutwa na Bunduki moja aina ya Shortgun yenye namba za usajili       TZCAR 356460 ikiwa na risasi saba ndani ya magazine.
Kamanda Sirro alisema pia zilikamatwa pikipiki tatu katika eneo la tukio zenye namba T769 CJW,MC.423ASH na MC982ASG pamoja na simu za mkononi nane za aina mbalimbali ambazo walikuwa wakizitumia kufanyia uhalifu.
 
Katika tukio jingine, wananchi wenyehasira kali wamemuua kwa kumpiga mawe mtu adhaniwaye kuwa ni jambazi katika eneo la Buguruni jijini dare s salaam.
Kamanda Sirro alisema jambazi huyo alipopekuliwa alikutwa  na silaha aina ya AK47 yenye namba M73B1-130887 ikiwa na magazine yenye risasi 13 ambayo ilikuwa ikitumiwa na wahalifu.
Alisema mafanikio hayo yametokana na oparesheni kabambe ya kuwasaka na kuwakamata majambazi wa kutumia silaha pamoja na uhalifu mwingine ikiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wanaishi na kufanya shughuli zao za kila siku bila hofu yoyote.

No comments: