Wednesday 24 June 2015

Mhe. Makinda ameahirisha kikao cha bunge kutokana na kifo cha mbunge wa Geita

Mhe. Makinda ameahirisha kikao cha bunge kutokana na kifo cha mbunge wa Geita Mhe Donald Max.
Spika wa bunge Mhe.Anna Makinda ameahirisha kikao cha bunge kutokana na kifo cha mbunge wa jimbo la Geita kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mhe Donald Kelvin Max kilichotokea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili juni 23 mwaka huu.
Akiahirisha kikao cha bunge Mhe.Makinda amesema marehemu amekuwa akiugua kwa muda mrefu hali iliyopelekea kulazwa hospitalini kwa kipindi kirefu ambapo amesema taratibu za mazishi zinafanywa na anatarajiwa kuzikwa jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi ya Jun 27.
Aidha wakizungumzia kifo cha marehemu Donald mMx, baadhi ya wabunge wamesema marehemu alikuwa ni mcheshi na mwenye kuelewana na wenzake kwa kipindi alichowahi kuhudhuria vikao vya bunge.

No comments: