Tuesday 16 June 2015

Polisi waokoa wasichana waliokuwa katika kiwanda cha kuuza watu

Polisi wavamia “kiwanda cha kuuza watoto” NigeriaPolisi waokoa wasichana wajawazito 9 katika kiwanda hicho nchini Nigeria

Afisa wa polisi katika mji wa Enugu Ebere Amaraizu ,amefahamisha kuwa wamevamia ‘kiwanda cha kuuza watoto’ mwishoni mwa juma,na kuwaokoa wasichana wadogo wenye mimba takriban 9, na mkumtia mbaroni mkurugenzi wa kiwanda hicho bwana Ikechukwu Onoh.
Afisa huyo amesema kuwa "wasichana wenye ujauzito 9 wameokolewa na wapo chini ya ulinzi wetu,"
Afisa amesema kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikiendesha shughuli zake katika jengo binafsi ambapo mmiliki anashukiwa kuwa ni daktari .
Afisa huyo pia alitaarifu kuwa "tutamshitaki kwa kosa la jinai baada ya kitengo cha makosa ya jinai kumaliza uchunguzi wake katika kesi hiyo,"
Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi jioni, mtuhumiwa alidai kuwa alikuwa na leseni ya kufanya kazi katika hospitali ya wazazi lakini alishindwa kuonyesha hati yoyote kuweza kujitetea.
Mmoja wa wasichana hao Happiness Mbaonu,amesema kuwa "tumekuwa tukilazishwa kubeba mimba kwa kubakwa na watu tusio wajua kisha baada ya kujifungua anachua watoto na kutupatia pesa na mahitaji mengine".

No comments: