Friday 26 June 2015

Serikali yakili kushindwa kudhibiti wahamaiji haramu Kyerwa na Karagwe mkoani Kagera.

Viongozi wa vyama vya kisiasa, maafisa uandikishaji na kamati za ulinzi na usalama wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera zimekili kushindwa kudhibiti wimbi la watu wanaosadikiwa kuwa wahamia haramu kutoka nchi ya Burundi, Rwanda na Uganda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura BVR wakishawishi baada ya watendaji wa serikali za vijiji, vitongoji na mawakala kuwapatia rushwa ya fedha na mifugo.
Wamebainisha hayo siku chache baada ya kukamilika kwa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura BVR katika mkoa wa Kagera ambapo wilaya ya Kyerwa imevuka lengo kwa kuandikisha watu wengi zaidi wakiwemo wahamiaji haramu zaidi ya 4000 huku wilaya ya Karagwe ikiandikisha kwa asilimia 97 na kubainisha kwamba wahamiaji haramu walioweka makazi katikati ya mapori na misitu ya hifadhi ya taifa walivamia zoezi la BVR kwa lengo la kujiandikisha kinyume cha sheria za nchi.
 Baadhi ya wanasiasa wamesema kuwa wimbi la wahamiaji haramu katika wilaya zilizopo mipakani halitaisha endapo serikali isipobadilisha mfumo wa utendaji katika maeneo ya mipaka ya nchi ambapo takwimu zinaonyesha kila siku wilaya ya Kyerwa na Karagwe watu 30 kuingia nchini kwa njia za panya.
 
Wakijibu malalamiko hayo kaimu mkuu wa wilaya ya Kyerwa Bw. Josephat Kakuru amesema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 12128 waliohifadhiwa katika kijiji cha Katera na Kihinda kwa lengo la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

No comments: