Monday 29 June 2015

Wanajeshi 60 wa Burundi wauawa na al shabaab

Wanajeshi 60 wa Burundi wauawa SomaliaWanajeshi 60 wa Burundi wauawa na al shabaab, taasisi za kiraia zalazimisha kuahirishwa kwa uchaguzi ili kuomboleza
Wanajeshi 60 wa vikosi vya kulinda amani nchini Somalia kutoka Burundi wauawa katika shambulio lililoendeshwa na wanamgambo wa al shabaab.
Kutokana na shambulio hilo wanaharakati wa asasi za kiraia wametoa wito kwa serikali kuahirisha tarehe ya uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Jumatatu Juni 29 ili kuomboleza vifo vya wanajeshi hao waliouawa na wanamgambo wa al shabaab.
Wanamgambo wa al shabaab walilijinasibu kuendesha shambulio Ijumaa na kuwauwa wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani na kuwauwa wanajeshi 60 kutoka Burundi Chabili kusini mwa Somalia.
Kanali Reverien Ndayambaje alithibitisha kuuawa kwa wanajeshi hao katika kituoa cha redio ya taifa mjini Bujumbura.
Pacifique Nininahazwe mmoja wa wanaharakati katika asasi za kiraia zinazopinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza aliandika katika akaunti yake ya Facebook kuwa badala ya kufanya uchaguzi ni vema kuomboleza vifo vya mashujaa waliouawa Somalia.
Serikali ya Bujumbura haijafahamisha lolote na kukemea vikali shambulio hilo la kigaidi lenye nia ya kuendelea kuyumbisha usalama nchini Somalia.
Ifahamike kuwa zaidi ya wanajeshi 6,000 kutoka Burundi wamo miongoni mwa vikosi vya kulinda amani nchini Somalia tangu mwaka 2007.

No comments: