Tuesday 23 June 2015

Wanaovalia suruali za kubana waonywa

Suruali ndefu zinazobana zina madhara
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 35 alilazimika kutolewa ndani ya suruali ndefu aina ya Jeans, baada ya miguu yake kuvimba kupita kiasi.
Hayo ni kwa mjibu wa jarida la Neurology, ambalo huandika habari kuhusu upasuaji.
Alichuchumaa kwa muda mrefu sana ili kuondoa bidhaa ndani ya kabati alipokuwa akijiandaa kuhama nchini Australia.
Ilipofika jioni, miguu yake ilikuwa imekufa ganzi na akashindwa kutembea.

Madaktari waanamini kuwa mwanamke huyo alipatwa na maradhi yanayojulikana kama compartment syndrome, ambayo yalisababishwa na suruali yake ndefu yenye kubana mno.
Ugonjwa huo ni mbaya sana na husababishwa na kujuja kwa damu na kuvimba kwa misuli.
Tatizo hilo lilimfanya mwanamke huyo kuteguka na kuanguka na akashindwa kuinuka. Alisalia ardhini kwa saa kadhaa.
Alipofikishwa katika Hospitali ya Royal Adelaide, sehemu ya chini ya miguu yake ilikuwa na uvimbe m'baya.
Ingawa miguu yake ilikuwa na joto na damu ilikuwa ikisambazwa vyema, misuli yake ilikuwa haina nguvu na ilikuwa imeshapoteza hisia.
Madaktari wengine wamesema kuwa wamepokea visa kadhaa ambapo wagonjwa wamelalamikia kudungwa dungwa pamoja na kuganda kwa mapaja, baada ya kuvalia suruali zinazobana.

No comments: