Friday 19 June 2015

Yanga yakanusha kumtimua Jerri Muro

Ktibu mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Toboroha (kushoto) akifafanua jambo (kulia) ni Afisa habari wa klabu hiyo Jerry Muro
Ktibu mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Toboroha (kushoto) akifafanua jambo (kulia) ni Afisa habari wa klabu hiyo Jerry Muro
Kufuatia taarifa kuzagaa mtaani kwamba, afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro kafutiwa kibarua chake kwenye klabu hiyo ya Jangwani, uongozi wa timu hiyo umeamua kulitolea ufafanuzi jambo hilo ili kuondoa utata na maswali mengi yanayoulizwa na mashabiki wa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu uliopita.
Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, hakuna ukweli wowote juu ya jambo hilo na kuongeza kuwa Jerry Muro bado ni afisa habari wa Yanga na ni mfanyakazi halali wa klabu hiyo na hakuna kikao kilichoitishwa kuchukua uamuzi huo.
“Hakuna ukweli juu ya jambo hilo, Jerry bado ni afisa wa habari na mahusiano na ni mfanyakazi wa Yanga, na hicho kikao si dhani kama kilifanyika maana mimi ndiye ninaeitisha vikao na sijaitasha kiako cha hivyo”, amesema.
“Nimeshangaa hata mimi kwasababu nimeona kwenye ‘groups za WhatsApp’ jana, nikasema hizi taarifa zinapotoka wakati mwingine siyo yeye. Nimeshawahi kuongea wakati mwingine unakuta taarifa zimeandikwa kwenye blogs, sasa sijui huyu mtu aliyeandika yeye taarifa amezitoa wapi”, alifafanua.
“Mashabiki wa Yanga waelewe kwamba, Jerry Muro bado ni mtumishi wa Yanga na bado ataendelea kuwahabarisha habari za Yanga. Tunajaribu kuangalia na kuchunguza chanzo cha hiyo habari ni nini”, Tiboroha  alimaliza.
Awali, kulikuwepo na taarifa zilizo zangaa kwenye mitandao ya kijamii (social networks) kwamba afisa habari wa Yanga Jerry Muro ametimuliwa kunako klabu hiyolakini habari hizo hazikwenda ndani zaidi na kusema sababu zilizopelekea Yanga kumtimua Muro.

No comments: