Sunday 5 July 2015

Azam kutangaza ligi kuu ya England kwa kiswahili sasa

Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga nchini kurusha ‘live’ mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.

Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema. 

“Tunafanya juhudi kubwa ili tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika kutupa haki ya matangazo hayo, tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.
“Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi yetu ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika ubora wa hali ya juu zaidi,” alisema Tido.

Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao matangazo ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.

No comments: