Tuesday 14 July 2015

Mwanamuziki mashuhuru 50 Cent amewasilisha stakabadhi za kuonyesha kuwa amefilisika


Senti za 50 Cent zamalizika; ajitangaza kufilisikaMwanamuziki mashuhuru 50 Cent amewasilisha stakabadhi za kuonyesha kuwa amefilisika

Mwanamuziki Curtis James Jackson maarufu kama 50Cent amefilisika. 50 Cent alipoteza dola milioni 5 katika kesi iliyowasilishwa na mwanamke mmoja aliyemshtaki kwa kusambaza video yake ya ngono.
50 Cent alipata umaarufu mkubwa baada ya kuzindua albamu yake ya “Get Rich or Die Trying” katika mwaka wa 2003.
50 Cent mwenye umri wa miaka 40 aliwahi kuuza albamu milioni 30 na pia aliwahi kushinda tuzo ya Grammy
50 Cent alipata mafanikio makubwa katika biashara kama ilivyokuwa katika muziki huku akipiga hatua kubwa alipouza kampuni yake ya maji VitaminWater kwa Coca-Cola katika mwaka wa 2007.
50 Cents amejisajili kupata hifadhi kupitia kifungo cha 11 ambacho kitamkinga dhidi ya mashirika na watu wanaomdai hadi atakapoweza kurekebisha hali yake ya kifedha.
Wakili wa 50 Cent William A Brewer alisema kuwa biashara ya mwanamuziki huyo bado zitaendelea

No comments: