Tuesday 7 July 2015

Raia wa Sudan auawa Libya, machafuko yaendelea

Raia wa Sudan auawa Libya, machafuko yaendeleaHali nchini Libya bado si shwari, mapigano yanaendelea katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Tripoli.
Habari za karibuni kabisa zinasema kuwa, raia mmoja wa Sudan ameuawa katika mapigano yanayoendelea mjini Tripoli.
Mtandao wa habari wa Libya al Mustaqbal umeripoti kuwa, mwili wa Omar Othman Hussein, raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 50 umepelekwa kwenye kituo kimoja cha matibabu mjini humo. Raia huyo wa Sudan ameuawa kwa kupigwa risasi kusini mwa Tripoli.
Serikali ya Libya imeshindwa kuyapokonya silaha makundi ya wanamgambo baada ya kupinduliwa utawala wa Kanali Muammar Gadafi.
Nchi za Magharibi zinalaumiwa kwa kuitelekeza Libya baada ya nchi hizo kufanya uharibifu mkubwa nchini humo wakati wa kampeni za kuupindua utawala wa Muammar Gadafi na kuacha silaha za kila namna zikiwa zimezagaa mikononi mwa makundi ya watu ambao kila mmoja anataka kuwa na ushawishi mkubwa zaidi nchini humo.

No comments: