Tuesday 7 July 2015

Rais Kikwete akijiandikisha kupiga kura

Zaidi ya watanzania milioni kumi na moja katika milioni ishirini na tano waliokusudiwa wamejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa mashine za BVR licha ya changamoto kadha wa kadha zilizo jitokeza.
Akisoma taarifa ya zoezi hilo mbele ya raisi Jakaya Kikwete, aliyeungana na watanzania wa mkoa wa Pwani kwenye kujiandikisha, mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu damiani lubuva,amesema taayari watanzania zaidi ya milioni kumi na moja wamejiandikisha katika mikoa kumi na tatu huku matarajiwa yakiwa ni watanzania milioni 24 wakitarajiwa, huku mikoa kumi na moja ikiwa imesalia kukamilisha zoezi hilo.
Raisi Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa watanzania waliojitikeza kujiandikisha katika kijiji cha Msoga Bagamoyo mkoani Pwani, kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi lililoanza kwenye mkoa huo, na kuipongeza tume kwa kuendelea na zoezi hilo licha ya kugubikwa na changamoto kadha wa kadha na kutoa wito kwa watanzania kuacha kulalamika mara baada ya uchaguzi bila ya kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura.
 
Baadhi ya wananchi wa Msoga waliojitokeza kujiandikish wameelezea changamoto ya huduma ya umeme kwaaajili ya matumizi ya mashine za BVR, ambapo wamesema watashirikiana kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa huku mbunge wa jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewaomba wananchi kujitokeza kujandikisha na kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba.

No comments: