Sunday 5 July 2015

Uzinduzi wa bwawa la kuvulia Pweza, Ras mzingo. Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani

 NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe:Mohammed Said Mohammed, akizungumza jambo na watendaji wa Wizara hiyo, wakati wakati walipokuwa wakiangalia eneo linalotaka kuvunwa Pweza huko Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani.


 MRATIB wa Jumuiya ya Sanaa ya Elimu ya Ukimwi na Mazingira kisiwa Panza (JSEUMA)Juma Ali Mati, akizungumza na mmoja kati ya wageni walioshuhudia uvunaji wa Pweza katika eneo la Kisiwa Panza.

 NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe:Mohammed Said Mohammed,mwenye suti katikati akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa bwawa la kuvulia Pweza katika Ras mzingo na Ufunguo huko Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani


 WANANCHI mbali mbali wa kisiwa Panza wakielekea baharini, kuvua Pweza mara baada ya kuzinduliwa kwa eneo lao la Ras mzingo na Ufunguo, ambalo lilikuwa limefungwa kwa muda wa Miezi Mitatu.



 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongoza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe:Mohammed Said Mohammed, katikati akiangalia wananchi wanavyovua Pweza mara baada ya kuzindua eneo la Uvunaji wa Pweza katika Ras Mzingo na Ufungu huko Kisiwa Panza.

 MMOJA wa wavuvi akirudi kuvuwa Pweza mara baada ya eneo lao la ufugaji wa Pweza kufunguliwa huko kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani.


 BAADHI ya wafanyakazi wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Pemba, wakimuangalia Pweza aliyevuliwa katika eneo la ufugaji lililofunguliwa huko Kisiwa Panza

WATOTO wakimtoa Pweza kwenye shimo lake mara baada ya kubaini kuwemo kwa Pweza katika shimo hilo, huko katika eneo la Ufugaji wa Pweza lililofunguliwa huko kisiwa Panza.

No comments: