Friday 24 July 2015

Vidal kutua Bayern Munich ya Ujerumani


Vidal kuelekea Bayern MunichBayern Munich yatangaza kuafikiana na Juventus kwa ajili ya usajili wa Vidal

Kiongozi wa kilabu ya Bayern Munich nchini Ujerumani Karl-Heinz Rummenigge, ametangaza kufanya makubaliano na kilabu ya Juventus kwa ajili ya usajili wa kiungo wa kati Arturo Vidal.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya Bayern Munich, Rummenigge alithibitisha kuafikiana na Juventus pamoja na Vidal kuhusu usajili wake
.

Rummenigge aliongezea kusema kwamba usajili wa Vidal umesalia hatua ya ukaguzi wa afya na kutia saini mkataba ili kukamilika na kuweza kuanza mazoezi na timu yake mpya wiki ijayo.
Tangu kusajiliwa na Juventus mwaka 2011, Vidal amefanikiwa kubeba taji la Seria A kwa mara ya 4 mfululizo na kucheza fainali ya UEFA Champions League mwaka 2015.
Vidal pia aliingia kwenye kurasa za historia ya Chile baada ya kushinda kombe la Copa America la mwaka 2015 na timu ya taifa.

No comments: