Saturday 25 July 2015

Wadau wataka tume ya uchaguzi kuongeza mudawauandikishaji wapiga kura Dar es Salaam

Kutokana na zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR mkoa wa Dar es Salaam kugubikwa na matatizo lukuki vyama vya siasa na wadau wa siasa wameitaka tume kuongeza mida pamoka na kuhakikisha kila kituo kina kuwa na mtaalamu wa komputa.
Zoezi hili likiwa limeingia siku ya tatatu jijini hapa huku idadi kubwa ya watu wakiwa hawajaandikishwa kwa madai ya ubovu wa mashine na waandikishaji ambao siyo wataalamu kumepelekea vyama hivyo vya siasa na wadau kuzungunzia hali hiyo kama wanavyoelezea.
Baadhi ya waandikishaji wamelalamikia mazingira magumu wanayofanyia kazi kutokana na baadhi ya wananchi kuwafanyia vurugu pale mashine zinapoharibika katikati ya zoezi huku wakilalamikia ubovu wa mashine zilizoongezwa.
Akijibu malalamiko ya changamoto hizo pamoja na suala la kuajiri watu wasiokuwa na utaalamu msimazi wa zoezi hilo ambaye ni mkurugenzi wa manispaa ya Ilala mbali na kukukiri kupokea malalamiko hayo ameiomba tume ya uchaguzi kuongeza wataalamu wa komputa huku akielezea utaratibu uliotumika kupata waandikishaji.

No comments: