Sunday 5 July 2015

Watu 9 wafariki baada ya jengo la kiwanda kuporomoka

9 wafariki baada ya jengo la kiwanda kuporomokaWatu 9 kati ya 51 waliokuwa kiwandani wafariki baada ya jengo la kiwanda hicho cha viatu kuporomoka nchini China

Wafanyikazi 51 waliripotiwa kuwa katika kiwanda hicho cha viatu wakati ajali hiyo ya ilipotokea. Wafanyikazi wote waliweza kuondolewa kutoka kwenye jengo hilo ila 9 kati yao waliaga dunia walipokuwa hospitalini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua watu 9 walifanikiwa kuondoka huku wengine 42 wakiokolewa na kikosi cha waokoaji kilichofika katika kiwanda hicho. Shughuli za uokoaji zilianza baada ya ajali hiyo kutokea mwendo wa saa kumi unusu jioni mpaka saa saba unusu usiku.
Uchunguzi ungali unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

No comments: