Tuesday 4 August 2015

Kiwanda cha mbu chaanzishwa China

Kiwanda cha mbu chaanzishwa ChinaMbu wa kiume kukuzwa kiwandani kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa kidindapopo

Wanasayansi wa China wameanza kukuza mbu wa kiume kiwandani wanaobeba bakteria kwa ajili ya kuangamiza mbu wengine wanaosababisha ugonjwa wa kidingapopo (dengue).


Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la China Daily, kiwanda hicho cha mbu kilichoundwa kwenye bustani moja ya kisayansi iliyoko mkoani Guangdong, kitaweza kukuza mbu milioni 10 wa kiume kila wiki.
Mbu hao watakuwa wakidungwa bakteria aina ya Wolbachia inayopatikana ndani ya wadudu wengi.
Baadaye mbu hao wa kiume watakaobeba bakteria hiyo watafunguliwa na kuachiliwa kupeperuka kwenye kisiwa cha Shenzhen chenye ukubwa wa kilomita 3 za mraba.
Kwa namna hiyo, bakteria iliyodungwa ndani ya mbu wa kiume itaweza kuangamiza mbu wa kike punde tu watakapojamiiana.
Mbinu hii inatarajiwa kupunguza idadi ya mbu kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.

No comments: