Saturday 15 August 2015

Lema na Mbatia watoa onyo Kali kwa Jeshi la Polisi


Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Godbles Lema amelilaumu jeshi la polisi Mkoani arusha kwa kujaribu kumzuia  msafara wa aliyekuwa waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Nne  na Mtia nia wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Chadema na UKAWA  kuwasili katika viwanja vya mkutano wa kumtambulisha Mh. Edward Lowasa kwa wananchi wa Arusha kama mgombea ambaye atapeperusha bendera ya chadema na Ukawa
Polisi waliwazuia wanachama wa Chadema na Ukawa ambao waliandamana na msafara wa Mh. Lowasa kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mkoan Kilamanjaro KIA, walipofika maeneo ya jimbo la Arumeru mashariki mji mdogo wa USA River karibu na Mto nduruma walikuta jeshi la polisi wakiwa wameweka vizuizi na kuanza kurusha mabomu ya machozi kuwatawanyisha wanachama wa Ukawa walioandamana na Lowasa.
Lema aliendelea kusema  “serikali na jeshi la polisi wanajaribu kuwaogopesha wananchi ili ccm waweze kuiba kura uchaguzi ujao “ Pia atoa salamu kwa IGP wa Arusha  “ Kama amewafundisha wanajeshi wake kuuwa basi yeye kajifunza kutembea akiwa maiti “
Lema akizungumzia swala la Jeshi la Polisi la Mkoa wa Kilimanjaro kumzuia Lowasa kwenda kumzika aliyekuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi  Mzee Kisumo  Alisema  haoni sababu ya maana ya lowasa kuzuiliwa kwenda msibani kwani haijawahi tokea duniani mtu akazuiliwa kwenda msibani  bali anahisi ni woga wa Rais Jakaya Kikwete kuwa atafunikwa na Lowasa katika msiba huo.
Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia nae awaonya jeshi la polisi kwa kuwaasa mkuu wa jeshi la Tanzania Mangu kuwa kama wataendelea kuwaonea wananchi kwa kuwapiga mabomu ovyo ovyo basi wasubirie mahakama ya ICC kuwatia mbaroni
Licha ya kuwaasa wakuu wa jeshi la polisi amemwaga sifa kwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa kusimamia Mkutano wao kwa makini na bila Uonevu wa aina yoyote  

No comments: