Sunday 16 August 2015

Maeflu wajitokeza Kumlaki Lowasa Arusha

Maelfu ya wananchi wa ndani na nje ya mkoa wa Arusha wamejitokeza kumpokea na kumsikiliza mgombea urais wa CHADEMA kupitia UKAWA na waziri mkuu wa zamani Mh.  Edward Lowasa huku wakishuhudu wanachama wa (CCM) na viongozi akiwemo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh.Laurence Masha.
Wengine waliojiunga na CHADEMA ni pamoja na katibu wa CCM wa wilaya ya babati  Bw,Daniel Porokwa,Mwenyekiti wa UWT,wa wilaya ya karatu  bi fabiola  manimo  katibu wa UWT wa wilaya ya Siha,na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa  Arusha kwa zaidi ya miaka 20 Mh.Yona Nnko.
 
Pia naye Mwenyekiti wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha Bw.Robson Naitinyiku,aliyegombea Ubunge wa jimbo la Simanjiro na kushika nafasi ya pili  Bw.Lenana Lenganasa,Diwani wa kata ya Ruvu Remiti wilayani Simaniro Bw,Siyoi Solomoni sumari na kiongozi mkuu wa ukoo wa ukoo wa nanyaro kutoka Arumeru  Mashariki.
 
Baada ya kazi ya kuwapokea wanachama wapya kukamilika viongozi wa ngazi  mbalimbali wa UKAWA akiwemo muasisi wa CHADEMA Mzee Edwin Mtey wakatoa salam   huku wakiendelea kuwataka watanzania kupokea mabadiliko na kuhakikisha kuwa  yanafanyika kwa amani.
 
Ukafika wakati wa mgombea urais wa CHADEMA kupitia umoja wa UKAWA Mh.Edward  Lowasana mgombea Mwenza Mh.Duni Haji ambao wameendelea kuwataka wananchi   kudumisha umoja na ushirikiano ili waweze  kushinda uchaguzi na kupata nafasi  ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayowakabli wananchi.

No comments: