Tuesday 4 August 2015

Mh.Lowasa ameridhiwa kuwa mgombea rasmi wa Ukawa.

Hatimaye mkutano mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema umeridhia jina la Edward Lowasa kuwa mgombea wa nafasi ya urais huku Bw Juma Duni Haji akipitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya makamo wa rais huku Maalim Seif Mahadi akipitishwa kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar.
Ni tambo za ushindi za Edward Lowasa alizozitoa dakika chache baada ya kupitishwa na mkutano mkuu wa Chadema kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Ukawa na kuvunja minongon iliyokuwa imetanda kuwa Ukawa isingefikia hatua hiyo.
 
Katika hutuba yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu Lowasa amesema anaamini kwa ushirika imara wa Ukawa wataweza kushinda viti vingi vya ubunge na nafasi ya urais huku akijinasibisha kuwa nguvu, nia na uweza wa kufanisha ushindi wa zaidi ya silimia 80 kwa nafasi ya urais.
 
Kwa muda mrefu amekuwa akinyoshewa kidole kuwa huenda akavunja muungano endapo atafanikiwa kuwa rais wa Zanzibar, lakini anasema muungano wa Tanzania utakuwa imara zaidi chini ya uongozi wa serikali ya Ukawa.
 
Awali akifungua mkutano mkuu wa Chadema mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kwani ni dhahili sasa safari ya uhakika imewadia.
 
James Mbatia ni moja ya viongozi wa Ukawa ambapo amevitaka vyombo vya ulinzi nchini kuhakikisha haviegemei upande wowote hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu, mkutano mkuu wa Chadema uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhulia na viongozi mbalili wa ndani na nje ya nchi pia umewapokea na kuwakabidhi kadi baadhi ya vigogo wa CCM wakiongozwa na mwenyekiti wa wenyeviti wa miko ya CCM Bw Mgana Msindai.

No comments: