Saturday 15 August 2015

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa vibaya katika ajali mkoani Geita.

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha gari mbili za mizigo na basi la abiria mali ya kampuni ya Sabuni Express katika kijiji cha Lubambangwe wilaya ya Chato mkoani Geita wakati dereva wa basi akijaribu kukwepa kugongana uso kwa uso na gari la mizigo hali iliyomsababisha kupalamia gari bovu lililoengeshwa barabarani ili kunusuru maisha ya watu.

Ajali hiyo imetokea katika  kijiji cha Lubambangwe nje kidogo ya mji wa Chato ambapo basi la Sabuni Express lenye namba za usajili T275 AZG likitokea mji mdogo wa mugaza kuelekea jijini Mwanza limepata ajali mbaya katika barabara ya buzirayombo kyemirwa baada ya kugongana na magari mawili ya mizigo aina ya Scania na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wenguine 30 kujeruhiwa vibaya ambapo baadhi ya majeruhi wamevunjika miguu na mikono huku mama mmoja mwenye watoto watatu aliyenusulika kifo katika ajali hiyo akikatiza safari na kurudi nyumbani kwake.
 
Akizungumza na ITV mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Chato Dr.Pius Buchukundi amesema kuwa amepokea majeruhi 31 kati yao mmoja akafariki dunia wakati akitibiwa huku majeruhi wawili wakizidiwa na kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi na kwamba majeruhi 20 wametibiwa na kuruhusiwa ambapo wagonjwa tisa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Chato na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
 

No comments: