Thursday 6 August 2015

Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba amejiuzulu.

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kikongwe hapa nchini.
 
Baada ya minongono ya kutaka kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa kile kilichodaiwa ni maelewano hasi na baadhi ya wakurugenzi wa chama hicho sasa ni rasmi.
 
Prof Lipumba aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka 1999 kuhusu mchakato wa katiba amesema kwa sasa haoni kama UKAWA utafanikisha upatikanaji wa katiba bora itakayoweza kukidhi  tunu za taifa, utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji, msomi huyo wa mashuhuri wa masuala ya uchumi nchini amesema katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi atajikita zaidi katika kuandaa ushauri wa mambo mbalimbali yanayopaswa kutekelezwa na serikali ijayo ambapo baada ya uchaguzi atajikita katika masuala ya kitafiti pekee.
 
Bw Jusa Ismail ni naibu katibu mkuu wa CUF Tanzania Zanzibar ambapo anakiri ofisi ya katibu mkuu kupokea taarifa za kujiuzulu mwenyekiti wa chama hicho makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam wanachama wa CUF walikuwa na mitazamo tofauti kuhusu taarifa hiyo ya kujiuzulu mwenyekiti wao.
 
Prof Ibarhimu Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari ambao hata hivyo haukuhusisha kiongozi yeyote wa chama cha wananchi CUF.

No comments: