Monday 23 November 2015

Baada ya Madrid Kuchapwa na Barcelona benzema ajikuta akihudhuria mazoezi mwenyewe


Benzema 2
Mshambuliaji Karim Benzema jana Jumapili alitokea pekee kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Madrid kufanya mazoezi baada ya kocha Rafael Benitez kuwapa ofa ya mapumziko wachezaji wa kikosi cha kwanza siku ya Jumapili kutokana na kipigo cha goli 4-0 kutokana kwa mahasimu wao Barcelona.

Benzema 3
Karim Benzema aliamua pamoja na kupewa ofa ya kupumzika, kutokea mazoezini huku akifanya mazoezi na kikosi cha pili sanjari na baadhi ya wachezaji wakubwa kama Arbeloa.
Benzema 1
Real Madrid ilipokea kipigo hicho kikubwa kutoka kwa Barcelona cha mabao 4-0 magoli yakifungwa na Luis Suarez (2), Neymar pamoja na Iniesta.
Mechi hii ilikua ni ya kwanza ya El Classico kwa kocha Rafael Benitez huku akitakiwa kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Shaktar Donestic Jumanne hii huku wachezaji wakianza mazoezi Jumatatu hii.
Benzema

No comments: