Wednesday 25 November 2015

Rubani wa Urusi aokolewa Syria

Rubani wa Urusi aokolewa Syria
Urusi inasema kuwa msaidizi wa rubani wa ndege ya kijeshi iliyodunguliwa na Uturuki hapo jana ameokolewa na kurejeshwa katika kambi yao ya kijeshi iliyoo Syria.
Urusi inasema kuwa afisa huyo yuko katika hali njema katika kambi ya kijeshi ya Lattakia.
Wizara ya ulinzi nchini Urusi inasema kuwa rubani mwingine na mwanajeshi aliyeshiriki katika operesheni ya kwenda kuwaokoa marubani hao wa ndege iliyodunguliwa nao waliuawa.
 
Ubalozi wa Urusi na taarifa kutoka kwa serikali ya Syria zinasema kuwa rubani huyo aliokolewa na wanajeshi wa Syria
Ubalozi wa Urusi na taarifa kutoka kwa serikali ya Syria zinasema kuwa rubani huyo aliokolewa na wanajeshi wa Syria na anarudishwa kwenye kambi ya jeshi la urusi eneo la Lattakia huko Syria.
Moscow inasema kuwa operesheni nchini Syria zitaendelea kuwakabili wapiganaji wa Islamic State na makundi mengine ya kijihadi.
Aidha Urusi imesema kuanzia leo ndege zinazoelekea kutekeleza operesheni za mashambulizi dhidi ya makundi ya kijihadi zitapewa ulinzi mkali na ndege za kivita.
Vilevile mitambo ya rada ya Urusi itatumika kuimarisha ulinzi wa angani katika maeneo ya mipakanai ya Syria.
Mitambo ya rada ya Urusi itatumika kuimarisha ulinzi wa angani katika maeneo ya mipakanai ya Syria.
Mitambo hiyo itawekwa katika kambi ya kijeshi ya Urusi iliyoko Lattakia.
Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.
Hakikisho hilo la rais Obama linafwatia hatua ya Uturuki kuidungua ndege ya Urusi karibu na mpaka wa Syria.

Umoja wa mataifa na muungano wa kujihami ya nchi za Maghraibu NATO wamewataka Urusi na Uturuki kutuliza hasira zao

No comments: