Sunday 13 December 2015

21 wafariki baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye hospitali moja ya vichaa nchini Urusi

Moto wazuka kwenye hospitali ya vichaa Urusi21 wafariki baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye hospitali moja ya vichaa nchini Urusi

Watu 21 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye hospitali moja ya vichaa iliyoko Voronezh, kusini magharibi mwa Urusi.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na wizara ya maafa na misaada ya dharura nchini Urusi, miili ya watu 19 ilipatikana kwenye eneo la tukio, huku wengine wawili wakiripotiwa kufariki wakati wa matibabu.
Watu wengine 55 pia wameweza kuokolewa na kuondolewa kutoka kwenye hospitali hiyo, huku baadhi yao wakiwa na majeruhi madogo ya kuunguzwa na moto huo.


Chanzo cha moto huo bado hakijabainishwa na uchunguzi umeanzishwa na bodi ya upelelezi ya Urusi.

No comments: