Tuesday 29 December 2015

Hiddink: Chelsea waonyeshe hamu dhidi ya Man Utd

WatfordChelsea walitoka sare 2-2 mechi dhidi ya Watford Jumamosi
Kaimu meneja wa Chelsea Guus Hiddink amesema timu yake inafaa kuonyesha hamu ya kutaka kushinda dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford leo.
Vijana hao wameshinda mechi moja pekee kati ya tano zilizopita, nao United wameshindwa mara tatu mfululizo ligini.
Chelsea walitoka sare 2-2 na Watford Jumamosi mechi ya kwanza Hiddink akiwa kwenye usukani baada ya Jose Mourinho kufutwa.
Mholanzi huyo amesema: "Mechi yoyote kati ya Chelsea na Manchester United ni kubwa lakini hii ni ya kipekee bila shaka.”
"Natumai tutaweza kuonyesha hamu ya kutaka kushinda kama tulivyofanya sehemu kubwa ya mechi (dhidi ya Watford).”
  • LVG: Naweza kuondoka mwenyewe Man United
Klabu hiyo ya Stamford Bridge itamkosa mshambuliaji Diego Costa ambaye haruhusiwi kucheza baada ya kuonyeshwa kadi ya tano ya manjano Jumamosi.
United huenda nao wakabadilisha kikosi cha kuanza mechi baada ya kushindwa 2-0 na Stoke City Jumamosi.
Kwenye mechi hiyo, nahodha wao Wayne Rooney alianza akiwa benchi kwa mara ya kwanza tangu Januari 2014.

Chelsea v Manchester United

Takwimu muhimu

8
Mechi ambazo Chelsea wameenda bila kushindwa na United ligini na katika kombe
5
Wachezaji ambao wamepewa kadi nyekundu mechi sita za ligi kati ya Chelsea na United
  • 6 Mechi za EPL ambazo Chelsea wameshinda Old Trafford, ni zaidi ya timu nyingine
Matokeo mabaya kwa United yamezidisha shinikizo kwa meneja Louis van Gaal ambaye baada ya mechi hiyo alisema anaweza kuamua kuondoka kwenye klabu hiyo.
Alipoulizwa iwapo atakuwa bado anasimamia timu hiyo dhidi ya Chelsea, alisema: “Mtahitaji kusubiri na kuona yatakayojiri, lakini nafikiri hivyo (kwamba atakuwa bado kwenye usukani) Ninahisi uungaji mkono kutoka kwa kila mtu katika klabu.”

No comments: