Thursday 17 December 2015

Maelfu waandamana kupinga serikali ya Jacob Zuma nchini Afrika Kusini

Maandamano ya kumpinga rais Zuma Afrika KusiniMaelfu waandamana kupinga serikali ya Jacob Zuma nchini Afrika Kusini

Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini walifanya maandamano hapo jana katika miji mikubwa ya Afrika Kusini kwa ajili ya kumpinga rais Jacob Zuma.
Waandamanaji hao waliokusanyika katika mitaa ya miji ya Johannesburg, Pretoria, Cape Town na Port Elizabeth, walimshutumu Zuma kwa madai ya ufisadi na kuzorotesha uchumi wa nchi.
Maandamano hayo yaliongozwa na kiongozi wa zamani wa muungano wa biashara Zwelinzima Vavi aliyemlaumu Zuma kwa kumbadilisha waziri wa fedha mara mbili ndani ya wiki moja.
Mnamo tareheh 9 Desemba, Zuma alimfuta kazi aliyekuwa waziri wa fedha Nhlanhla Nene na kumteua David van Rooyen kuziba pengo hilo.
Ndani ya wiki hiyo, Zuma baadaye akamuondoa David van Rooyen na kumteua Pravin Gordhan kuwa waziri mpya wa fedha.

No comments: