Friday 11 December 2015

Tanzania yapata maabara ya kuchunguza Ebola

TanzaniaTanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya kuathiriwa na vijidudu vingine.

Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee kusini mwa Jangwa la Sahara zenye maabara ya aina hii ambayo itakuwa msaada mkubwa pia kwa nchi za jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR Dokta Mwele Malecela, amesema maabara hii ina umuhimu kwa kuwa itawezesha kufanyika kwa uchunguzi kwa urahisi na haraka zaidi, hata katika maeneo yaliyo na ugumu kufikiwa.
Maabara Maabara hiyo inatarajiwa kurahisisha uchunguzi wa magonjwa hatari
Changamoto ambayo ilionekana wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi ni wahudumu kutofika kwa urahisi kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi wa haraka kutokana na umbali na miundo mbinu mibovu.

No comments: