Sunday 13 March 2016

Rais Magufuli kateua Wakuu wapya wa mikoa… yumo na Paul Makonda,

Magufuli awateua wakuu 13 wapya wa mikoa
Rais wa Tanzania amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa leo na ikulu ya rais.
Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliohudumu katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Mussa Ibrahim Iyombe.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika ikulu, Gerson Msigwa, Viongozi hao wote walioteuliwa wataapishwa katika hafla maalum itakayoandaliwa jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa tatu asubuhi jijini Dar es salaam.
Orodha ya wakuu wa mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
Afisa Mkuu wa Mkoa




  1. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zelote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14. Jordan Mungire Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16. Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara.
  17. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18. John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19. Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21. Joel Nkaya Bendera – Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23. Rehema Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24. Mhandisi Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa – Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Gerson Msigwa, wakuu wote wa mikoa walioteuliwa wataapishwa Jumanne tarehe 15 March 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Dar es salaam.















































No comments: