Thursday 14 April 2016

Zaidi ya shilingi Bilioni 900 zatumika kwa ajili ya miradi itakayo zindulia na Mwenge.

Mwenge wa Uhuru unanarajiwa kuwashwa Kitaifa mkoani Morogoro mapema April18 Mwaka huu ambapo zaidi ya bilioni Miatisa na Milioni Miatatu zimetumika kwa matumizi ya miradi 41 ambayo itazinduliwa huku mingine ikiwekwa jiwe la Msingi.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa sare za nguo za kuvaa watoto kwenye Mwenge zilizo tolewa na benki ya NMB kanda ya Mashariki mkuu wa mkoa wa Morogoro Stephan Kebwe amesema maandalizi ya Mwenge yako vizuri na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya wa mejipanga kuhudhuria uzinduzi huo.
 Zaidi ya shilingi Bilioni 900 zatumika kwa ajili ya miradi itakayo zindulia na Mwenge.
Kwaupande wake meneja wa NMB kanda ya Mashariki Nazareth Lebby amesema wametoa mabosi 20 ya nguo za kuvaa vijana katika Mwenge yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 34 ikiwa ni mchango wao katika kufanikisha kuwasha mwenge mkoani Morogoro.
 
Aidha katika hatua nyingine benki ya NMB tawi la wami mkoani Morogoro wametoa msaada wa madawati 50 katika shule ya sekondari lupanga ambapo shule hiyo ilikuwa na uhaba wa madawati 90 na kwa kupata hayo yatasaidia kupunguza usumbufu wa wanafunzi kukosa pakukaa.

No comments: